RADIO HURUMA. (TANGA DIOCESE MULTIMEDIA COMPANY LTD (TDMCL))

KANISA KATOLIKI TANGA

Radio Huruma ilianza matangazo yake tarehe 24 Desemba 2007

Hii ni Radio inayomilikiwa na kanisa Katoliki Tanga.

Matangazo ya Radio Huruma yalianza na urushaji wa ibada ya misa ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas, ibada iliyofanyika katika kanisa Kuu la Mtakatifu Anthony wa Padua, Cathedral Church Chumbageni Tanga. Ibada hii iliongozwa na Mhashamu Askofu Anthony M. Banzi Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga. Siku hadi siku Radio Huruma imezidi kuimarika na kuwa chombo muhimu kwa wakazi wa Tanga kwa upande wa kupata Elimu na Burudani.

MALENGO YA RADIO HURUMA (RH)

Malengo ya Radio Huruma ni;
kuwaamsha wakazi wa Tanga kifikra, hasa katika mambo yanayohusu maendeleo yao na pia kutangaza neno la Mungu.
TBC Taifa, Radio ya Taifa, hutangaza habari zinazohusu taifa zima. Ni mara chache sana TBC Taifa hutangaza habari za Tanga na kwa ufupi sana.
Tanga yapo mengi ambayo yanatakiwa kutangazwa. Radio Huruma itaangalia kwa undani kila siku mambo yanayohusu Tanga, shughuli za wakazi wa Tanga na kuimiza ujenzi wa uchumi kwa kila mkazi wa Tanga.
Radio Huruma hutoa elimu kwa wasikilizaji wake, kuwahabarisha, kuwaburudisha na kuhamasisha umoja na amani, upendo, haki sambamba na kulitangaza neno la Mungu. Kwa kufanya hivyo Kanisa la Tanga linakamilisha ile kazi inayofanywa na serikali katika mapambano ya umasikini, ujinga, maradhi na kuwaandaa watanzania kuwa watu wema.
Radio Huruma inajitahidi kujenga jamii yenye kuzingatia misingi ya haki, amani na upendo.

KITUO KILIPO:
Kituo cha utangazaji kipo katika jiji la Tanga, katika Kanisa kuu la Jimbo Chumbageni Tanga katika jengo lijulikanalo "PWANI HOUSE"

MASAFA YETU:
Radio Huruma inasikika karibu nusu ya eneo lote la Mkoa wa Tanga na baadhi ya mikoa jirani, ambayo ipo karibu na mnara wetu wa kurushia matangazo.